0
Yakiwa yamebaki masaa machache kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Brazil,shamrashamra zinazidi kuongezeka hasa kwa mashabiki wa soka kote Duniani kuanza kujiandaa kuelekea nchini Brazil,Huku balozi zikijaa mashabiki wa nchi mbalimbali kwa ajili ya maandalizi.Moja ya vitu vinavyofanya mvuto wa Kombe la Dunia nchini Brazil kupamba moto ni Idadi ya wachezaji mastaa wataoziwakilisha nchi zao kama Cristiano Ronaldo,Rooney,Suarez,Costa,Neymar,Messi,Tores,Samuel Etto na Didier Drogba,vingine vinavyovutia zaidi ni hasa mji wa Brazil unavyosifika kwa kuwa vichaa wa soka,fukwe nzuri zinazorembeshwa na warembo wazuri wa kibrazil. Kama Shabiki wa Soka lazima kuna timu unayoishabikia katika michuano ya mwaka huu nchini Brazil inayojumuisha mataifa 32 yaliyofuzu kwenye michuano hiyo,Licha ya Dosari kutokea kwa baadhi ya mastaa kukosa Kombe la Dunia kutokana na majeraha na wengine nchi zao kushidwa kufuzu,moja ya wachezaji wanaokosa ni Zlatan Ibrahimović,Frank Ribery,Radamel Falcao,Riccardo Montolivo ,Rafael van der Vaart na pia kuna mastaa wengine walioenguliwa mapema na makocha kutokana na kushuka kiwango au kukosa nidhamu kama Kaka,Nasir,ronaldinho na Carlos Teves.Je timu yako ni ipi??

Post a Comment

 
Top