Sababu kubwa za mvua kuathiri miundombinu ni
udhaifu na uongozi mbovu wa serikali ya Dar es salaam. Naelekeza haya matatizo
Dar kwa sababu Moshi Kilimanjaro hayapo.
Ktk maisha yangu, kitu ninachokichukia kupita
vyote ni kuona mtu mwenye akili zake anatupa takataka ovyo
Mtu ananunua miwa harafu anatafuna huku
anatupa ovyo ovyo. Mtu anatupa anavyojisikia kutupa apendavyo. Takataka za
majumbani zinatupwa kwenye madaraja ovyo.
Viongozi wanakimbilia kwenye kuzuia pikipiki
kuingia mjini wkt hatari ipo kwenye utupaji wa takataka ovyo.
Ukichunguza madhara ya utupaji taka, sidhani kama
serikali inaweza kushindwa kuzuia hili tatizo. Binafsi naona ni uzembe wa hali
ya juu.
Leo tunaona wananchi hao hao nyumba zao
zimejaa maji. Mitaro imeziba, maji yanabadili njia.
Tuanze na tuchukue hatua. Sema NO na
"NO" kwenye mkono unao ruhusu kutupa takataka.
Kwa mfano angalia picha zifuatazo,,,
Serikali ya Jiji la Dar es Salaam ndo tatizo,inaongoza kwa mazoea???????????amkeni usingizini mtunge sheria na kuzisimamia ni marufuku mtu kutupa taka ovyo ukidhibitika umetupa taka ovyo fine,, plus sero sku mbili tosha kabisa kwa kuanzia.
Post a Comment