Abuja;
Rais mteule wa Naijeria Muhammadu Buhari kashutumu madai Boko
Haram ya kuwa kundi la kidini kuwa ni upotoshwaji, Rais mteule ameeleza kwamba
atapambana vikali dhidi ya wanamgambo wa Kiislam.
"Wadanganyifu hawa waitwao Boko Haram wanaweza kushindwa na
kutokomezwa kabisa kwa kuangamiza ngome zao za mafunzo,huu ni mradi wao tu
wenywewe wamejiajiri sasa wanatumia dini, Hakuna dini inaruhusu mauaji ya
watoto katika mabweni ya shule, katika masoko na maeneo ya ibada.,"
Alisema.
"Hawana dini inayowafanya wawe hivyo, hawa ni magaidi na sisi
tutakabiliana nao kama tunavyo kabiliana na magaidi."
Buhari, alishinda uchaguzi wa rais mwezi uliopita kwa ahadi ya
msimamo mkali dhidi ya Boko Haram, ambao ni waasi inakadiriwa watu takribani
elfu 15 wameshaa uawa tangu 2009 na kuanza zaidi ya million moja na nusu 1,500,000
bila makazi.
mtawala huyo wa zamani wa kijeshi alimtuhuhu mpinzani wake Rais
Goodluck Jonathan kwa kushindwa kuongoza katika kukabiliana na tishio la
usalama wa taifa ilo.
Hakuna kitu kibaya ambacho mtu anaweza kufanya kama kukataza
watoto kupata elimu,hiyo itakuwa kuwaharibia watoto maisha ya baadae.
Buhari ambaye atatawazwa kuwa Raisi rasmi mei 29,
ametahadharisha kuwa hawezi kuahidi kuwa atawaokoa na kuwarudisha salama watoto
219 waliotekwa nyara zaidi ya mwaka sasa.
Lakini yeye ameahidi kusaidi maeneo yaliyo kumbwa na vurugu na
kunyimwa haki za kijamii na uchumi yaendelee na mipango ya maendeleo.
Taarifa hii ilitolewa na chama chake cha All Progressives
Congress (APC)
Post a Comment