John ni
kijana mwenye umri wa miaka 30.
Ana shahada
ya uzamili (Masters) ktk
masuala ya
Usimamizi wa biashara, na
kwa sasa
anafanya kazi kama Mkurugenzi
wa fedha
kwenye shirika moja la
kimataifa
hapa nchini.
Hajaoa bado,
lakini ana nyumba mbili
nzuri za kuishi
hapa jijini. Moja Mbezi
Beach na
nyingine Kimara.. Ana gari 2 za
kutembelea na
3 za biashara.. Anamiliki
duka moja la
nguo Kariakoo na jingine la
simu Mlimani
city.. Ni mcha Mungu,
mpole na
mtanashati.. Ni miongoni mwa
vijana
waliofanikiwa kimaisha.
John ana
rafiki yake aitwae Michael..
Huyu ni Afisa
Mtendaji mkuu (CEO) wa
Shirika moja
la ndege hapa nchini. John
na Michael
wamekua marafiki kwa muda
mrefu.. tangu
utotoni..
Wamekua
pamoja, wamesoma pamoja
tangu
chekechea hadi chuo kikuu. Hata
masomo yao ya
juu (masters) walisoma
pamoja
Marekani licha ya Michael kupata
ufadhili
Australia, lakini alikataa kwenda
ili tu
akasome na John Marekani.
Walipendana
kama mapacha licha ya
kuwa hawakuwa
ndugu wa damu..
Ukimkosea
John umemkosea Michael and
its vice
versa.!
Waliitwa
mapacha walipokua shuleni kwa
namna
walivyopendana. Kila mmoja
alimheshimu
mwenzie na kila mmoja
alijitahidi
asimkwaze mwenzie..
Kila mmoja
amefanikiwa kutokana na
juhudi za
mwenzie.. upendo wao ulikua
wa kweli
kutoka kwenye vilindi vya mioyo
yao..
Walimpenda Mungu na wote
walikua
viongozi wa jumuiya za vijana
makanisani
mwao.
Baada ya
kuona wamefanikiwa kimaisha
John
akashauri watafute wenzi wa
maisha...that
means waoe.. Michael
akasema
anahofia kuoa kwa haraka kwani
anaweza
kupata mke atakayeharibu
urafiki wao..
Mke asiyejua walikotoka na
hivyo kuleta
mfarakano baina yao...
Akamshauri
John wasubiri kwanza hadi
WAKATI WA
BWANA ULIOKUBALIKA..
John
hakumuelewa Michael kbs, na
akadai tayari
ana mchumba na
anampenda
sana.. Michael akamuuliza
kwa muda gani
wamekuwa pamoja, John
akajibu miezi
6.
Michael
akasema Miezi 6 haitoshi
kumchunguza
mwenzi wa maisha lakini
John
akasisitiza anampenda...
Mipango ya
harusi ikafanyika na Michael
akachagua
kuwa mwenyekiti wa kamati ya
harusi ya
John.. Lengo lake likiwa
kusimamia
harusi ya rafiki yake na
kuhakikisha
inafanikiwa.
John
akamshauri Michael "tafadhali nawe
tafuta mwenzi
uoe ili usiwe mpweke. Ni
dhahiri sasa
nitakua karibu zaidi na mke
wangu kuliko
wewe. Majukumu ya
kifamilia
nayo yatanibana, hivyo tafuta
mwenzi ili
upunguze upweke..."
Michael
akajibu "Nimemuomba Mungu
anipe mke
atakayenifaa.. Bado nasubiri
jibu lake.
Siwezi kuoa ili tu niepuke
upweke,.maana
ndoa ni zaidi ya kuondoa
upweke..
Nahitaji mwenzi wa maisha,
sihitaji mtu
wa kuniondolea upweke.."
Siku moja
John akiwa katoka Michael
akampigia
simu kuwa yupo nyumbani
kwake. John
akamuomba amsubiri maana
yuko mbali
kidogo ila atarudi.
Mke mtarajiwa
wa John nae alikua
nyumbani
kwake, hivyo John akamshauri
Michael apige
story na shemeji yake hadi
atakaporudi.
Lakini John
aliporudi nyumbani
hakumkuta
Michael, akamkuta mchumba
wake analia..
alipomuuliza kulikoni
akasema
Michael alijaribu kumbaka...
John akawaka
kwa hasira... kwa kuwa
alimpenda
sana mchumba wake na kwa
kuwa
hakumkuta Michael nyumbani
akaamini
maneno ya mchumba wake.
Akiwa
amechanganyikiwa akaendesha gari
kwa kasi
kwenda kwa Michael. Ile kufika
akamkuta
Michael kajilaza kwenye sofa.
Lakini kabla
hajamuuliza chochote,
akampiga
kichwani na chupa ya mvinyo
aliyokua
ameshika mkononi... Michael
akaanguka na
kuzirai..
Akakimbizwa
hospitalini ambako
ilionekana
amepata athari kubwa ndani
ya kichwa
hivyo alihitaji upasuaji..
John akiwa
amefura kwa hasira akarudi
nyumbani kwa
mguu na kuiacha ile gari
kwa Michael,
maana alipewa zawadi na
Michael siku
ya birthday yake.. hivyo
akamrudishia
zawadi yake maana aliona
mtu
aliyejaribu kumbaka mchumba wake
hawezi kumpa
zawadi.
Kwa kuwa
hakuwa na gari aliweza kuingia
hadi ndani
bila mchumba wake kumsikia
wala
kumuona... Alipofika akamkuta
anaongea na
simu "yes Jenny
nimemkomesha..
atajuta kukukataa...Nim
emwambia John
kuwa alitaka kunibaka,
John akawaka
hasira na kwenda
kumfuata...
najua huko ni kivumbi na
jasho na
urafiki wao utaisha leo shosti..."
Alipomaliza
kuongea na simu na kugeuka
akamuona
John.. Akapanick maana
hakutegemea...
John
akamwambia usiseme lolote maana
nimesikia
yote.
Kumbe Jenny
alikua rafiki yake mchumba
wa John.. Na
alipenda kuolewa na
Michael
lakini Michael alimkataa ili
kulinda
urafiki wake na John.. sasa ile
hasira ya
kukataliwa ndo wakapanga
kuwafarakanisha..
John alipojua
ukweli akajilaumu sana kwa
maamuzi ya
haraka aliyochukua.. akiwa
mnyonge,.na
majuto moyoni akakimbia
hospitalini
ili akamuombe Michael
msamaha.
Alipofika
akakutana na nesi akamzuia..
John akapaza
sauti huku akibubujikwa na
machozi
"tafadhali naomba niruhusiwe
nikamuombe
Michael msamaha.. Najua
amepoteza
fahamu na hawezi kunisikia.
Lakini
naamini nafsi yake itanisikia na
kunisamehe
kwa ukatili niliomtendea..
Ooh Michael
my friend urafiki wetu wote
nimeshia
kukupeleka ICU..Nisamehe
Michael
sikujua..."akalia kwa uchungu
John.
Mara daktari
akatokea. John kwa shauku
akamuuliza
"dokta Michael
anaendeleaje??"
Daktari
akamuangalia John kwa huruma
kisha akasema,
"Nasikitika kukujulisha
kuwa Michael
amefariki dakika chache
zilizopita
baada ya damu nyingi kuvujia
kwenye
ubongo.."
Kisha
akaongeza "tumejitahdi kwa kadri
ya uwezo wetu
kuokoa maisha yake lakini
imeshindikana.."
John
akakamatwa na kutupwa gerezani
anakotumikia
kifungo cha maisha..
MORAL OF THE
STORY..!
Kuwa makini
unapotafuta mwenzi wako
wa maisha.
Wengi huharibu mahusiano
yao na rafiki
zao, ndugu zao au wazazi
wao kisa
wameoa/kuolewa.
Usiruhusu
mke/mume awe chanzo cha
uadui kati
yako na ndugu zako, wazazi au
rafiki zako.
Ukiona
mke/mume ni chanzo cha uadui
na ndugu zako
ujue huyo mke/mume ana
roho ya
mfarakano (spirit of confusion).
Pilli,
unapopata tatizo kwenye mahusiano
kuwa na
subira.. Usiharakie kufanya
maamuzi.
Mara zote
maamuzi ya haraka
humgharimu
mtu baadae. Ona John ktk
umri mdogo wa
miaka 30, anaenda
kumalizia
gerezani maisha yake yote
yaliyobaki
hapa duniani.
Mali zake,
elimu yake, cheo chake,
heshima yake
na vyote alivyovijenga
maishani ni
kazi bure, just for a single
mistake.
Bila shaka
huko gerezani alipo
anatamani
siku zirudi nyuma ili afanye
maamuzi
mbadala lakini haiwezekani
tena... Itz
over and out..!!
Mungu
akubariki unayesoma ujumbe
huu. Kama
umeoa/kuolewa amuondolee
mwezi wako
Spirit of Confusion, na kama
hujaoa upate
mke/mume asiye a spirit of
confusion.
Upate mtu
atakayewapenda rafiki zako,
ndugu zako na
wazazi wako na
kuwathamini..
Kumbuka
"asiyewapenda wa kwao ni
mbaya kuliko
asiyeamini.."
Hivyo muombe
Mungu umpate
atakayewapenda
wa kwenu.
Stay
blessed.!!
Post a Comment