Baada ya kuwaza sana...nimegundua jiji lote la Dar ni
sehemu ya bahari. Bado historia haijanithibitisha ila naamini mwanzoni
mwa karne ya 16 jiji hili lilikuwa bahari...Kutokana na kukua na
maendeleo ya Dunia unaoendana na uharibifu wa mazingira ulipelekea maji
ya bahari kusogea na kurudi nyuma taratibu kwa zaidi ya karne
2...kuondoka kwa maji hayo kuliacha ardhi ikiwa tupu na baada ya miaka
mingi baadae binadamu wakalikuta eneo lililo pembezoni mwa bahari. Jamii
hiyo ya watu kutoka bara wakaweka makazi eneo hili na kuanzisha familia
na kutokana na kujitenga kwao kwa miaka mingi, wakajikuta wanatengeneza
mila na desturi zao ndipo wakajiita jamii ya Wazaramo. Wazaramo
limetokana na mtazamo wa kusema jamii yao ilitengwa...hivyo
ilidharauliwa..ndipo wakasema 'Waza + ramo'
Uthibitisho wa Nadharia hii.
1.Kuwepo na mafuriko kila mahali linalolikumba jiji hili ni jambo linaleta usahihi wa mtazamo wangu.
2.Kuwepo na vilima na miunuko iliyopo pembezoni mwa mkoa wa Dar es salaam kama vile Pugu,Mbezi n.k...miunuko ni sifa ya bahari.
3.Jiji la Dar es Salaam sehemu kubwa ni tambarare na hakuna udongo eneo lote la Dar ni michanga.
4.Kupitiwa kwa mwamba wa bahari ardhini....hii
inathibitishwa popote unapochimba kisima katika sehemu yoyote ya Dar
unapata maji.
Post a Comment