0

Akiongea na Viongozi wa vyama vya siasa juu ya mambo mbali mbali katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu,Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema ugawaji wa majimbo ya uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka 10.

Ugawaji wa majimbo utazingatia vigezo mbali mbali ikiwemo idadi ya watu,upatikanaji wa mawasiliano,hali ya kigeografia na vigezo vingine kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka 2010.


Post a Comment

 
Top