MATOKEO
YA UCHUNGUZI WA AWALI KUMHUSU NDUGU ELIAKIM
C. MASWI, KATIBU MKUU, WIZARA YA NISHATI NA MADINI
C. MASWI, KATIBU MKUU, WIZARA YA NISHATI NA MADINI
1.0
Utangulizi
1.1
Katika mkutano wake wa 16 na 17, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
pamoja na mambo mengine, lilijadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali iliyotokana na Taarifa ya Ukaguzi wa Akaunti ya Tegeta
Escrow uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
1.2
Baada ya majadiliano, Bunge lilipitisha maazimio kadhaa yaliyoelekezwa kwa
Serikali kwa ushauri na utekelezaji. Mojawapo ya maazimio hayo yalimtaja Ndugu
Eliakim C. Maswi, ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kuwa
amehusika kijinai au kimaadili katika miamala iliyotokea katika akaunti ya
Tegeta Escrow.
1.3
Wakati anahutubia Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam tarehe 22 Desemba, 2014,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema ifuatavyo:-
“Kuhusu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma,
anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. Hivyo, nimeshaelekeza
Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za
kinidhamu zitachukuliwa.”
1.4
Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zimeshughulikiwa katika ngazi mbili
tofauti. Amechunguzwa na Sekretarieti ya Maadili ya Umma, kisha baada ya hapo
alichunguzwa pia na Kamati ya Uchunguzi wa Awali iliyoundwa na mamlaka yake ya
nidhamu.
2.0
Sekretarieti ya Tume ya Maadili
2.1
Kifungu 18 (2) (c) na (3) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kinaipa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mamlaka na uwezo wa kuchunguza
tuhuma yoyote ya kuvunjwa kwa maadili ya uongozi wa umma yanayotawaliwa na
Sheria hiyo. Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zilizomo kwenye maazimio ya
Bunge zinatawaliwa na Sheria hiyo.
2.2
Katika kutekeleza majukumu yake, Sekretarieti ya Maadili ya Umma ilifanya
uchunguzi wa awali na kisha kumhoji Ndugu Eliakim C. Maswi tarehe 19 Desemba,
2014.
2.3
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma haijabaini kuwepo kwa maslahi
binafsi katika uamuzi uliofanywa na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini wa
kuruhusu fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow kutolewa. Aidha, hawakubaini
ukiukwaji wowote wa maadili ya viongozi wa umma uliofanywa na Ndugu Eliakim C.
Maswi. Waliona kuwa yote aliyoyafanya yalizingatia matakwa ya Sheria, ushauri
wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na ridhaa ya TANESCO. Hivyo,
Sekretarieti ya Maadili haikuona msingi wowote wa kuendelea na shauri la Ndugu
Eliakim C. Maswi, na wamelihitimisha.
3.0
Kamati ya Uchunguzi wa Awali ya Mamlaka ya Nidhamu
3.1 Kwa
mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002
(kama ilivyorekebishwa) Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu ya
Makatibu Wakuu.
3.2 Kwa
kuzingatia Azimio husika la Bunge, na kwa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Katibu Mkuu Kiongozi aliunda Kamati ya Uchunguzi wa Awali
dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
chini ya Kifungu cha 36 cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003
kinachotamka ifuatavyo:-
“Where it is necessary to institute disciplinary proceedings against a public servant, the disciplinary authority shall make preliminary investigations before instituting disciplinary proceedings.”
“Where it is necessary to institute disciplinary proceedings against a public servant, the disciplinary authority shall make preliminary investigations before instituting disciplinary proceedings.”
3.3 Kwa
mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni 35(2)(b) na Kanuni 37 ya Kanuni za Utumishi
wa Umma za mwaka 2003, Katibu Mkuu Kiongozi alimpumzisha Bwana Eliakim C. MASWI
kutekeleza majukumu yake ya kazi ya Katibu Mkuu ili kupisha uchunguzi wa awali.
Uchunguzi wa awali ulifanyika chini ya Kanuni ya 36 ya Kanuni za Utumishi wa
Umma zilizotajwa, pamoja na Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na.
8 ya mwaka 2002, kama ilivyorekebishwa.
3.4 Kwa
mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni zilizotajwa kwenye ibara 3.3 hapo juu, Katibu
Mkuu Kiongozi aliteua Kamati ya Uchunguzi wa Awali na kuipa Hadidu za Rejea
zifuatazo:
3.4.1Kubainisha
wajibu na madaraka halisi ya Katibu Mkuu, Wizaraya Nishati na Madini, kwenye
uendeshaji wa TANESCO kwa ujumla, na hususan kwenye kufungua, kuendesha na
hatimaye kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow.
3.4.2Kubainisha
na kupata maelezo ya kina juu ya kuhusika kwa Bwana Eliakim C. Maswi katika
mchakato na mtiririko mzima wa akaunti ya Tegeta Escrow, tangu kufunguliwa hadi
kufungwa.
3.4.3Kubainisha
na kupata maelezo ya kina iwapo kuna jambo lolote ambalo Bwana Eliakim C. Maswi
alilifanya au ambalo alipaswa kulifanya lakini hakulifanya, linalomstahilisha
achukuliwe hatua za nidhamu.
3.4.4Kubainisha
na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua yoyote ya mchakato na mtiririko wa
tangu kufunguliwa hadi kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow, Bwana Eliakim C.
Maswi alifanya jambo lolote linalodhihirisha matumizi mabaya ya mamlaka yake
kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa namna iliyosababisha
hasara ya aina yoyote ile kwa Taifa la Tanzania.
2.3.5
Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua yoyote tangu akaunti ya
Tegeta Escrow ilipofunguliwa hadi ilipofungwa, Bwana Eliakim C. Maswi
hakuchukua tahadhari ya kutosha kulinda maslahi ya umma na kusababisha kupotea
kwa fedha za umma kwa uzembe au matumizi mabaya ya madaraka.
2.3.6
Kubainisha iwapo kuna mahali popote katika mchakato wa akaunti ya Tegeta Escrow
ambapo Bwana Eliakim Chacha Maswi alifanya jambo lolote linaloashiria kitendo
cha kijinai, au kukiuka maadili ya viongozi wa umma.
2.3.7
Kuandaa taarifa ya uchunguzi wa awali kwa msingi wa Hadidu za Rejea zilizomo
humu na kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Taarifa hiyo, pamoja na mambo
mengine, ipendekeze hatua za kuchukuliwa kwa kila eneo ambalo Kamati itabaini
umuhimu wa hatua kuchukuliwa.
2.4
Mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi wa Awali
2.4.1
Kamati haijabaini kosa lolote ambalo linaweza kusababisha Ndugu Eliakim Chacha
Maswi, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, kufunguliwa mashtaka ya
kinidhamu kwa kukiuka Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 ikisomwa pamoja na
Kanuni zake za mwaka 2003 kwa kuruhusu Benki Kuu ya Tanzania kutoa fedha
zilizokuwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
3
Hitimisho la Uchunguzi wa Awali
3.1
Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili umebaini kuwa Ndugu
Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote ya kimaadili katika mchakato wa fedha za
akaunti ya Tegeta Escrow.
3.2
Hali Kadhalika Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Kamati ya Uchunguzi wa Awali
iliyoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi umebaini kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi,
“hakutenda au kuhusika na jambo lolote linaloashiria vitendo vya jinai au
kukiuka Maadili ya Viongozi wa Umma”.
3.3
Ushahidi wa vielelezo uliotolewa kwenye Sekretarieti ya Maadili na kwenye
Kamati ya Uchunguzi wa Awali umejitosheleza kuthibitisha kwamba Ndugu Eliakim
C. Maswi alitenda kazi yake kwa kiwango kinachoridhisha kwa kufanya mawasiliano
na mamlaka mbalimbali na kwa nyakati tofauti kwa lengo la kuhakikisha na
kujiridhisha kwamba kufungwa kwa Akaunti ya Tegeta Escrow kunafanyika kwa
usahihi.
3.4
Hakuna ushahidi wowote kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi alikuwa miongoni mwa
waliopata mgao wa fedha au fadhila yoyote kutokana na kufungwa Akaunti ya
Tegeta Escrow.
3.5 Kwa
nafasi yake ya mamlaka ya nidhamu Katibu Mkuu Kiongozi, ameridhika kuwa Ndugu
Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote aliyoyafanya katika mchakato wa akaunti ya
Tegeta Escrow yanayostahili adhabu. Hivyo, mchakato wa kinidhamu, kimaadili na
kijinai dhidi yake umefikia mwisho wake. Mwenye mamlaka ya uteuzi atatafakari
taarifa hizi na kuamua cha kufanya kuhusu ajira yake baadaye.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Mei, 2015
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Mei, 2015
Post a Comment