Prof anachambua pamoja na mambo mengine , madhaifu ya Zitto
Kabwe na kushauri apatiwe mda wa kujirekebisha aweze kuwa kiongozi wa kitaifa,
mapungufu hayo kwa maneno yake mwenyewe Proffessor:
Pengine udhaifu mkubwa wa Zitto kama kiongozi upo katika maeneo makubwa mawili.
Pengine udhaifu mkubwa wa Zitto kama kiongozi upo katika maeneo makubwa mawili.
Kwanza, ni kushindwa kupima maana na matokeo
mapana ya kauli zake kabla hajazitoa. Mara kadhaa Zitto amekuwa akitoa kauli
ambazo huacha ukakasi mkubwa katika jamii.
Kwa mfano, akiwa katika kampeni za ubunge
mwaka 2010 alitangaza kwamba katika awamu ijayo angerudi kugombea urais na siyo
ubunge tena.
Zitto alitoa tangazo hili huku akijua
kwamba chama chake kilikuwa na mgombea urais na kwamba kauli kama ile ingeweza
kupunguza imani ya wapiga kura kwa mgombea wa chama chake kwa kuonyesha kwamba
asingeshinda na pengine alikuwa hafai.
Pili, baadhi ya kauli za Zitto huonyesha
kwamba ni kiongozi anayechokozeka kirahisi.
Kwa mfano, alipomwagiwa ‘upupu’ na Tundu
Lissu mapema mwaka huu kwamba alikuwa amehongwa magari na Nimrod Mkono, Zitto
alitoa kauli ya haraka tata kwamba, yeye asingekufa kama alivyokufa Chacha
Wangwe (“Chacha died, I won’t”).
Hii ni kauli tata kwa sababu inatoa taswira
kwamba pengine Chacha Wangwe hakufa kwa ajali kama inavyojulikana bali aliuawa
na watu ndani ya chama chake.
Pili, kwamba yeye asingekufa kama Wangwe
inaweza kutoa taswira kwamba Zitto ana nguvu za ziada za kumkinga na kifo.
Eneo la pili la udhaifu wa Zitto lipo
katika mahusiano ya kimapenzi yasiyoeleweka kwa mtu mwenye dhamana ya uongozi.
Zitto amekuwa akihusishwa na wasichana kadhaa maarufu hapa nchini ambao maadili
yao kindoa yanatia shaka katika mazingira ya Kitanzania.
Inapokuja katika mahusiano ya kimapenzi,
Zitto hujisahau kabisa kwamba yeye ni kiongozi mkubwa katika jamii pamoja na
kwamba ana haki zake kama binadamu.
Pengine hili ndilo eneo ambalo Zitto
ameshindwa kujitofautisha na wanasiasa wenzake hapa nchini, ambao wengi wao nao
uadilifu wao katika eneo hili ni wa mashaka.
Hitimisho
Post a Comment